MZEE WA SPIDI 120 HATIHATI KUWAVAA COASTAL UNION

MZEE wa spidi 120 Tuisila Kisinda kuna hatihati ya kuanza kwenye mchezo wa kesho kutokana na kutokuwa fiti.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kesho Desemba 20,2022 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union.

Kwa mujibu wa Cedrick Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo huo isipokuwa Kisinda bado yupo kwenye matazamio.

“Mazoezi ya mwisho ya leo na namna atakavyoamka itatoa picha kamili ya yeye kuanza ama kutoanza kwa sababu hakuwa fiti asilimia 100.

“Ukweli ni kwamba tunajua mchezo wetu dhidi ya Coastal Union hautakuwa mwepesi tupo tayari,” amesema.

Yanga imetoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania inakabiliana na Coastal Union ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya KMC