>

NAMUNGO 0- 1 YANGA

JONATHAN Nahimana kosa moja alilofanya dakika ya 40 limekuwa ni faida kwa Yanga ambao walimtungua bao wakati huo.

Ni kazi ya Yannick Bangala ambaye alimaliza mpira uliotemwa na kipa huyo wakati akiokoa pigo la faulo iliyopigwa na Aziz KI.

Namungo wanacheza mchezo wa kujilinda wakiwa Uwanja wa Majaliwa kwenye mchezo wa leo.

Wamekamilisha dakika 45 bila kupiga shuti ambalo limelenga lango zaidi ya kuonekana kwenye mtego wa kuotea mara mbili kwa nyota wao Relliats Lusajo.

Yanga wamepiga mashuti mawili ambayo yamelenga lango na moja limezama kambani, ngoma ni nzito kwa Namungo huku Yanga wakiwa na furaha ndani ya dakika 45.