LEO Uwanja wa Majaliwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Namungo v Yanga unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku.
Timu hizo zimekutana mara sita ambapo ni mchezo mmoja Yanga ilisepa na ushindi Uwanja wa Mkapa na mechi tano waligawana pointi mojamoja.
Hizi hapa rekodi zao walipokutana kwenye msako wa pointi tatu namna hii:-
Rekodi za Namungo v Yanga kwenye ligi:-
15/3/2020, Namungo 1-1 Yanga
24,6,20220, Yanga 2-2 Namungo
22,11,2020, Yanga 1-1 Namungo
15,2,2021 Namungo 0-0 Yanga
20,11,2021, Namungo 1-1 Yanga
23,4,2022, Yanga 2-1 Namungo