Home Sports PUMZIKA KWA AMANI NYOTA WA MPIRA

PUMZIKA KWA AMANI NYOTA WA MPIRA

UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kuwa umempoteza shujaa ambaye alikuwa mchezaji wa timu hiyo.

Ni Graham Enock Naftari ambaye alikuwa mchezaji wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara Tanzania alitangulia mbele za haki Desemba Mosi.

Taarifa iliyotolewa na Ruvu Shooting ilieleza kuwa nyota huyo alipatwa na umauti akiwa kwenye matibabu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa moja ya shujaa ambaye walikuwa wanaamini kwamba atairejesha Ruvu Shooting kwenye reli ni pamoja na kiungo huyo.

“Mwanzo mwa msimu Ruvu Shooting wachezaji wake wapatao 11 walipata fursa ya kwenda kusoma kwa ajili ya kupata mafuzo ya kijeshi naye alikuwa miongoni mwao, tulikuwa tunaamini kwamba mzunguko wa pili watakaporudi wachezaji wote akiwa pamoja na yeye tutakuwa kwenye mwendo mzuri.

“Haijawa hivyo mapenzi ya Mungu yametimia. Alikuwa anauwezo wa kucheza nafasi mbili kwa umakini ni ile ya ushambuliaji ambapo alikuwa ni tegemeo pamoja na ile ya kiungo.

“Alijiunga na Ruvu Shooting mwaka 2018 wakati tulipokuwa tunafanya scout ya wachezaji Morogoro na alianza na timu ya vijana chini ya miaka 20, ilipofika 2020 alikuwa amezidi kidogo ule umri ambao ulikuwa unahitajika.

“Wakati huo kocha alikuwa ni Salum Mayanga aliona kipaji chake na kumpandisha kwenye timu ya wakubwa msimu wa 2020 na tulikuwa tunamtegemea,”.

Pumzika kwa amani

Previous articleMTAMBO WA KUMWAGA MAJALO YANGA KUPEWA DILI JINGINE
Next articleMOSES PHIRI NA FISTON MAYELE NGOMA NZITO