VINARA WA LIGI KUU BARA NDANI YA MTWARA

 BAADA ya ushindi ambao wameupata mbele ya Tanzania Prisons kikosi hicho kimeibukia Mtwara.

Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons mtupiaji akiwa ni Feisal Salum dakika ya 89 na kuipa ushindi timu hiyo.

Sasa Yanga ni vinara wa ligi wakiwa wamecheza mechi 14 n kibindoni wana pointi 35 wanakutana na Namungo ambayo imekusanya pointi 15 zote zikiwa zimecheza mechi 14.

Namungo imetoka kunyooshwa mabao 3-0 dhidi ya Singida Big Stars kwenye mchezo wao uliopita uliochezwa Uwanja wa Liti.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Desemba 7, Uwanja wa Majaliwa.

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Fiston Mayele, Kibwana Shomari, Bangala, Djum.