DAKIKA 15 ziliwatosha Azam FC kuiondoa nafasi ya pili Simba kwa kupata ushindi mbele ya Polisi Tanzania.
Uwanja wa Ushirika, Moshi umesoma Polisi Tanzania 0-1 Azam FC ikiwa ni bao la dakika ya 15 kupitia kwa mtambo wao wa mabao Ayoub Lyanga.
Hili linakuwa bao la kwanza kwa nyota huyo kufunga na kuipa pointi tatu Azam FC inayonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala.
Lyanga katoa pasi tano za mabao akiwa ni namba moja kwa mastaa wenye pasi nyingi za mabao.
Azam FC inafikisha pointi 35 na kukwea nafasi ya pili huku Simba ikishushwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 34 zote mbili zimecheza mechi 15.
Mpaka dakika 90 zinakamilika Polisi Tanzania ambao mchezo wao uliopita walipoteza kwa kufungwa mabaoa 1-3 dhidi ya Simba walikwama kupata pointi.