YANGA WAWAPIGISHA KWATA WAJELAJELA

MOJA ya mchezo bora uliokamilika kwa Yanga kuitungua Tanzania Prisons dakika ya 89 bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.

Prisons ambao wnanolewa na Patrick Odhiambo nidhamu ya kujilinda ilikuwa kubwa dakika 45 za mwanzo huku umakini kwenye safu ya ushambuliaji ukiwa ni mdogo kwao.

Pongezi kwa kipa wa Prisons Abel ambaye umakini wake kwenye kulinda lango umewapa ugumu Yanga kupata mabao mengi ambapo aliokoa michomo dakika ya 3,5,7,35,41 na kuifanya tmu hiyo kwenda mapumziko ikiwa haijafungwa.

Kwa upande wa ushambuliaji, Jeremia Juma atajilaumu kwa nafasi ambazo alikosa kwenye mchezo wa leo hasa kipindi cha kwanza.

Ni yuleyule, Zanzibar Finest Feisal Salum alipachika bao la ushindi na kuipa pointi tatu Yanga mazima ikiwa imeanza safari ya kukusanya mechi bila kufungwa.

Yanga inarejea kileleni ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 14 inaishusha Simba nafasi ya kwanza iliyokuwa imekusanya pointi 34 ikiwa imecheza mechi 15.