SUAREZ: INAUMA KUSEMA KWAHERI KOMBE LA DUNIA

STAA wa Timu ya Taifa ya Uruguay, Luis Suarez amesema kuwa inauma kusema kwaheri Kombe la Dunia.

Nyota huyo hakuwa na chaguo baada ya timu hiyo kuondolewa mazima kwenye hatua ya makundi licha ya kupata ushindi kwenye mchezo wa mwisho.

Uruguay waliinyoosha mabao 2-0 Ghana kwenye mchezo wa makundi na kukusanya pointi tatu lakini walikwama kusonga hatua ya 16 bora kutokana na tofati ya mabao ya kufunga na kufugwa.

Ni Korea Kusini ilipenya baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Ureno jambo ambalo wengi walikuwa hawajatarajia na kuifanya timu hiyo kufunga jumla ya mabao manne huku Uruguay ikiwa na mabao mawili.

Suarez amesema:”Kusema kwaheri kwa Kombe la Dunia inaumiza sana lakini tumeoondoka tukiwa na amani na kila kitu kuhusu nchi yetu,”.