PELE AWATOA HOFU KUHUSU AFYA YAKE

LEGEND kwenye ulimwengu wa soka ambaye anatajwa kuwa mchezaji bora wa muda woteraia wa Brazil Pele amewaomba mashabiki na wale wanaomfuatilia wasiwe na mashaka kuhusu afya yake.

Nyota huyo kupitia mitandao ya kijamii ameandika ujumbe ambao unaeleza kwamba anaendelea vizuri na matibabu anaamini atarejea kwenye ubora wake.

Pele alipelekwa hospitali ya Sao Paulo tangu Jumanne kutokana na kutokuwa fiti kwa afya.

Nyota huyo amesema:”Ninataka kila mtu ambaye anafuatilia uhusu mimi awe na utulivu, ninaendelea vizuri na ninapewa matibabu mazuri pia.

“Kwa namna ambavyo ninafuata maelekezo na matibabu ambayo ninapata nina amini nitakuwa imara na kurejea kwenye ubora, asante kwa kujali na asanteni sana,”.

Ni tatizo la kansa ambalo inaripotiwa kwamba anasumbuliwa nayo nyota huyo mwenye miaka 82.