NGOMA NZITO NYANKUMBU, NTIBANZOKIZA ALA UMEME

JASHO la wanaume kwenye msako wa pointi tatu Uwanja wa Nyakumbu limegotea kwa kila mmoja kusepana pointi mojamoja.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Geita Gold 2-2 Mtibwa Sugar.

Said Ntibanzokiza alipachika bao la kuongoza dakika ya 34 kwa mkwaju wa penalti na alitoa pasi moja ya bao kwa Juma Luizio dakika ya 45+4

Kwa upande wa Mtibwa Sugar wao pointi moja walisepa nayo kupitia kwa mabao ya Onesmo Mayanja aliyepachika bao mapema dakika ya 10 na lile la pili dakika za lala salama na staa wa Mtibwa Sugar, Adam Adam.

Hivyo nyota hawa kila mmoja amevuna kile ambacho amekipanda kwa muda wa kusaka ushindi wa dakika 90.

Mchezo wa leo nyota Ntibanzokiza alionyeshwa kadi nyekundu kipindi cha pili baada ya kumchezea faulo nyota wa Mtibwa Sugar.