MTAMBO wa mabao ndani ya Yanga Fiston Mayele kuanza kwake leo kikosi cha kwanza ni hatihati kwa kuwa hakufanya mazoezi na timu hiyo mwanzo.
Kwa mujibu wa kocha msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze alisema kuwa Mayele hakufanya mazoezi na wenzake hivyo mazoezi ya mwisho yataamua yeye kuanza kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.
Mayele mwenye mabao 10 kwenye ligi huenda asiaze kikosi cha kwanza akaanzia benchi mchezo wa leo.
Mbali na Mayele pia kinara wa pasi za mwisho ndani ya Yanga, Jesus Moloko mwenye pasi tatu za mabao naye kuna hatihati ya kuanza kikosi cha kwanza.
Mtambo mwingine wa kazi ni Dickson Job beki wa kati ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano huyu hatakuwa sehemu ya mchezo.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Mkapa, Desemba 4 saa 1:00 usiku.
Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 13 kinara ni Simba mwenye pointi 34 baada ya kucheza mechi 15.