TIMU ya taifa ya Argentin inatinga hatua ya robo fainali Kombe la Dunia Qatar kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Austaralia.
Kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa Uwanja wa Ahmad bin Ali mashabiki 45,032 walishuhudia burudani hiyo.
Ni mabao ya Lionel Messi ambaye alikuwa nyota kwenye mchezo huo alifunga dakika ya 35 na Julian Alvarez huyu alifunga kipindi cha pili dakika ya 57 kukamilisha maao mawili yaliyoipa ushindi timu hiyo.
Bao la Australia lilikuwa ni lakujifunga dakika ya 77 kupitia kwa E Fernandez kwenye mchezo huo.
Sasa Argentina inatarajiwa kumenyana na timu ya taifa ya Netherlands kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.