SINGIDA BIG STARS WATATU WATUPIA NA KUSEPA NA POINTI

MABAO matatu ambayo yameituliza Namungo FC ikiwa Uwanja wa Liti yamefungwa na nyota watatu ambao kwa nyakati tofauti wote waliwahi kucheza mitaa ya Kariakoo.

Ubao wa Liti Desemba 2,2022 ulisoma Namungo 0-3 Singida Big Stars na kuwafanya vijana wa Hans Pluijm kusepa na pointi tatu ugenini.

Ni Meddie Kagere alikuwa wa pili kufunga bao la pili dakika ya 76 na wa kwanza kufunga alikuwa Said Ndemla dakika ya 27.

Shukran kwa Amis Tambwe ambaye alifunga bao la tatu kukamilisha idadi hiyo kwa wakulima hao dakika ya 90+2.

Jithada za Namungo kusaka ushindi zilikwama licha ya kutengeneza nafasi kadhaa.

Ni bao la nne kwa Meddie Kagere msimu huu akiwa na uzi wa Singida Big Stars baada ya kusepa ndani ya kikosi cha Simba baada ya msimu wa 2021/22 kumeguka.