TUNISIA SAFARI IMEWAKUTA LICHA YA KUSHINDA

LICHA ya timu ya taifa ya Tunisia kutoka Afrika kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa kwenye mchezo wa makundi Kombe la Dunia, Qatar 2022 safari yao imegota ukingoni.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Ufaransa walianzisha wachezaji wake wengi nyota benchi kwa kuwa inaonekana kuwa mbinu ya benchi la ufundi ilikuwa ni kuwapumzisha mastaa wake.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Wahbi Khazir dakika ya 58 kipindi cha pili na kuwapa nguvu ya kuendelea kupambana mwanzo mwisho.

Kutoka kundi D, Tunisia walikuwa wanaomba sare kwenye mchezo wa timu ya Australia lakini haikuwa hivyo timu hiyo ilishinda.

Ushindi wa bao 1-0 ambao walipata Austaralia mbele ya Denmark unawafanya wafikishe pointi sita wakiwa nafasi ya pili na vinara wa kundi ni Ufaransa ambao wanaungana nao kwenye hatua ya 16 bora.

Staa wa Ufaransa Kylian Mbappe aliingia kipindi cha pili na kuongeza presha kwa upande wa ushambuliaji lakini alikwama kufunga.

Bao la Antoine Griezmann ambaye naye alianzia benchi lilikatiliwa na VAR jambo ambalo liliifanya Tunisia kushinda mchezo huo mgumu lakini wanarejea nyumbani wakiwa nafasi ya tatu na pointi zao ni nne.

Tunisia inavunja rekodi ya Ufaransa kutofungwa kwenye mechi za Kombe la Dunia ambapo rekodi zinaonyesha kuwa mara ya mwisho timu hiyo kufungwa ilikuwa ni mwaka 2014.

Ufaransa ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani kwenye na kwa sasa Ufaransa ni mabingwa watetezi wanatarajia kumenyana na Poland kutoka kundi C Jumapili.