MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO KUANZA NA KURUGENZI

MABINGWA watetezi wa Kombe la Azam Sports Federation, Yanga kwenye mchezo wao wa raundi ya Pili wataanza na Kurugenzi FC.

Yanga ni mabingwa watetezi ambao walitwaa ubingwa huo uliokuwa mikononi mwa watani zao wa jadi Simba.

Kikosi hicho kipo chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi akifanya kazi kwa ukaribu na Cedric Kaze ambaye ni msaidizi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kati ya Disemba 9-11 Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo Yanga watakuwa wenyeji wa mchezo huo.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliweka wazi kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa wanawaheshimu wapinzani wao wote.

“Wapinzani wetu wote ambao tunakutana nao kwenye mechi zetu tunawaheshimu na tunajua kwamba kila timu inahitaji kupata ushindi mbele yetu nasi tunajipanga kupata matokeo,”.