KOCHA KMC ATAJA WANAPOKWAMA

KOCHA Mkuu wa KMC, Hitimana Thiery amesema kuwa wanashindwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo wanacheza kutokana na wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza kutokuwepo kikosini.

KMC mchezo wake uliopita wa ligi ubao wa Uwanja wa Uhuru ulisoma KMC 0-0 Prisons na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Kocha huyo ameweka wazi anaamini wachezaji wake wakipona watakuwa kwenye mwendo bora kwa ajili ya kufikia malengo yao.

“Kweli matokeo ambayo tunapata sio mazuri hasa ukizingatia kwamba ambacho tunataka ni pointi tatu na ushindani ni mkubwa na hii inatokana na ukweli kwamba kuna wachezaji wa kikosi cha kwanza hawapo fiti,” amesema