WATATU SIMBA WAWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA

KWENYE orodha ya nyota watatu wa Simba ambao wameingia fainali ya kuwania mchezaji bora chaguo la mashabiki ndani ya Novemba kiungo Mzamiru Yassin jina lake limepenya pia.

Wengine wawili ambao anapambana nao ni pamoja na Shomari Kapombe ambaye ni beki wa kazi pamoja na kiungo mgumu Sadio Kanoute.

Kikosi hicho jana Novemba 27,2022 kilikuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania.

Kwenye mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 ikiwa ni ushindi mkubwa kuupata msimu huu wakicheza kwenye uwanja wa nje ya Dar.

Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ligi ina ushindani mkubwa na wachezaji wake wote wanajituma kusaka ushindi.