ANGALAU timu ya taifa ya Cameroon imepata matumaini ya kutinga hatua ya 16 bora Kombe la Dunia Qatar lakini itakutana na kigogo kizito Ijumaa dhidi ya Brazil.
Sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Serbia inawapa nguvu ya kupambana mchezo ujao licha ya kwamba walikuwa na nafasi ya kushinda mchezo wa leo.
Ni Jean-Charles Castelletto dakika ya 29 liliwapa uongozi Cameroon huku bao la usawa kwa Serbia likifungwa na Strahinja Pariovic dakika ya 45+1 na lile la pili likifungwa na Sergej Milinkovic-Savic dakika ya 45+3.
Bao la tatu kwa Serbia ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa kusepa na ushindi kwenye mchezo wa kundi G lilifungwa dakika ya 53 na Aleksandar Mitrovic.
Vincent Aboubakar alifunga bao la pili dakika ya 63 kwa Cameroon na lile la tatu lilifungwa na Eric Maxim Chaupo-Moling dakika ya 66 na kufanya ngoma iwe 3-3.
Sasa kazi kubwa kwa Serbia yenye pointi tatu, nafasi ya pili ni kusaka ushindi dhidi ya Switzerland Uwanja wa Lusail, Ijumaa huku Cameroon yenye pointi moja nafasi tatu muziki wao ni dhidi ya Brazil, Ijumaa.