MABINGWA watetezi wa Kombe la Dunia Ufaransa ni timu ya kwanza kutinga hatua ya 16 kwenye mashindano hayo makubwa nchini Qatar.
Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Denmark umeipa tiketi timu hiyo kutangulia mbele ikipewa nafasi ya kuendelea kuleta ushindani.
Katika Uwanja wa 974 ambao umejengwa kwa idadi hiyo ya makontena kwa Ufaransa staa wao Kylian Mbappe alipachika mabao yote mawili.
Kwenye kundi D kazi bado inaendelea licha ya Ufanransa kufanikiwa kukata tiketi ya kutinga 16 bora, Denmark ambao wapo nafasi ya tatu huku Tunisia wakiwa nafasi ya nne hawa wana pointi moja na Australia wao wana pointi tatu nafasi ya pili kwa atakayeshinda mchezo wake ana nafasi ya kusonga mbele.
Ni dakika ya 61 na 86 na anafikisha mabao matatu kwenye Kombe la Dunia mwaka huu na lile la Denmark lilipachikwa na Andreas Christensen dakika ya 68.