POLISI TANZANIA 0-2 SIMBA

WAKIWA Uwanja wa Ushirika Moshi, ubao unasoma Polisi Tanzania 0-2 Simba mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ni mabao ya dakika ya 32 kupitia kwa John Bocco na lile la pili ni mali ya Moses Phiri ambaye amefunga dakika ya 43.

Mchezo kwa sasa ni mapumziko ambapo dakika 30 za mwanzo ilikuwa kila timu inafanya shambulizi kwa mpinzani wake.

Polisi Tanzania wamekuwa na umiliki mzuri wa mpira huku wakimtumia mshambuliaji wao Vitalis Mayanga kutengeneza nafasi za ushindi.

Upande ambao yupo Gadiel Michael umekuwa ukitumiwa mara nyingi na Polisi Tanzania kuliandama lango la Aishi Manula.