FISTON Mayele amefikisha mabao 10 kwenye Ligi baada ya leo kutupia mabao mawili mbele ya Mbeya City.
yanga imesepa na pointi tatu jumlajumla za Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo alifunga bao la kwanza dakika ya 24 na lile la pili dakika ya 70.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya mechi 29 kwenye mechi za mashindano ya ndani bila kupoteza.
Inafikisha pointi 32 kibindoni baada ya kucheza mechi 12 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Pia kutokana na ushindi huo na kuifikia rekodi ya Arsenal, uongozi wa Yanga uligawa keki kwa mashabiki wake leo Uwanja wa Mkapa kwenye kila jukwaa.