>

UFARANSA WAPIGA 4G

MABINGWA watetezi wa Kombe la Dunia wamepindua meza kibabe na kusepa na pointi tatu mazima kwenye mchezo wa kwanza wa makundi dhidi ya Australia.

Austaralia wakiwa Uwanja wa Al Janoub mbele ya mashabiki 40,875 walianza kupata bao la kuongoza mapema dakika ya 9 kupitia kwa Craig Goodwin.

Ni Adrien Rabiot alipachika bao dakika ya 27, Olivier Giroud alipachika mabao mawili ilikuwa dakika ya 32,71 huku msumari mmoja ukipachikwa Kylian Mbappe alipachika bao dakika ya 68.

Rekodi zinaonyesha kuwa ni mashuti 23 walipiga Ufaransa kuelekea lango la wapinzani wao huku 7 yakilenga lango na ni mashuti manne walipiga Austaralia na moja pekee lililenga lango.