SENEGAL WAANZA KWA KICHAPO

 KUTOKA Afrika Senegal ilikwama kupata ushindi kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia baada ya kupoteza mchezo wa kwanza.

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa Al Thumama ulisoma Senegal 0-2 Uholanzi ambao walisepa na pointi tatu mazima.

Bila Sadio Mane kwenye mchezo huo dakika 45 za awali Senegal walipambana na kuelekea mapumziko wakiwa hawajafungwa na wao pia hawakufunga.

Kipindi cha pili dakika ya 84 ni Cody Gakpo alipachika bao la kwanza na Davy Klaasen dakika ya 90+9 alipachika bao la pili.

Ni mashuti 15 Senegal walipiga huku manne yakilenga lango wakati Uholanzi wao walipiga mashuti 10 na matatu yalilenga lango kwa timu hizo ambazo zipo kundi A.