BALE AWATIBULIA MAREKANI KOMBE LA DUNIA

BAO la nahodha wa timu ya taifa ya Wales, Gareth Bale dakika ya 82 kwa mkwaju wa penalti lilitibua hesabu za ushindi kwa timu ya taifa ya Marekani.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Al Rayyan ni kipindi cha kwanza Marekani ilipata bao la mapema ambalo liliwapa uongozi.

Dakika ya 36 staa wao Timothy Weah alipachika bao hilo ambalo liliwapa matumaini ya kusepa na pointi tatu.

Kwenye mchezo huo ni mashutu sita timu ya taifa ya Marekani ilipiga huku moja pekee lililenga lango na kwa upande wa Wales wao walipiga mashuti 7 na matatu yalilenga lango.

Ni kundi B wapo ambapo vinara ni England wenye pointi tatu kisha Iran wao wapo nafasi ya nnehawana pointi, Wales nafasi ya pili na Marekani nafasi ya tatu wakiwa na pointi mojamoja.