ULIMWENGU wa mpira umeshutshwa na matokeo ya leo kwenye mchezo wa Kombe la Dunia katika kundi C.
Wakati wengi wakiwapa matumaini Argentina yenye Lionel Messi kushinda ngoma iligeuka na wakapoteza mchezo huo.
Dakika 90 ubao wa Uwanja wa Lusail umesoma Argentina 1-2 Saudi Arabia ambao wamesepa na pointi tatu mazima.
Ni bao la Lionel Messi dakika ya 10 kwa mkwaju wa penalti lilikuwa pekee kwa timu hiyo huku Saudi Arabia wakipindua meza dakika ya 48 kupitia kwa Saleh AIshehri na lile la ushindi ni mali ya Salem Aldawsari dakika ya 53