MABAO 8 yamekusanywa leo kwenye mchezo wa Kombe la Dunia huko Qatar baada ya dakika 90 kukamilika.
Ubao wa Uwanja wa taifa wa Khalifa umesoma England 6-2 Iran kwenye mchezo wa kundi B.
Mabao ya Jude Bellingham dakika ya 35, Bukayo Saka dakika ya 43 na 62, Raheem Sterling dakika ya 45+1, Marcus Rashford dakika ya 71 na msumari wa mwisho ulipigwa na Jack Grealish dakika ya 89.
Msumari wa Grealish ulikamilisha idadi ya mabao 6 huku yale mawili kwa Iran yakifungwa na Mehdi Tarem dakika ya 65 na 90+13 kwa mkwaju wa penalti.