KIBWANA Shomari beki wa Yanga ameweka wazi kuwa alikuwa na nia ya kufunga jambo ambalo lilitokea baada ya dakika 90 kumeguka Uwanja wa Mkapa.
Novemba 17,2022 Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 Singida Big Stars na kuwafanya wasepe na pointi tatu mazima.
Watupiaji walikuwa ni wawili ambapo Fiston Mayele alitupia mabao matatu na kusepa na mpira wake alianza dakika ya 16akitumia pasi ya Jesus Moloko, dakika ya 27 kwa pasi ya Feisal Salum na dakika ya 56 kwa pasi ya Lomalisa.
Bao la Kibwana lilipachikwa dakika ya 48 kwa pasi ya Mayele huku Singida ig Stars waliokuwa wakipewa nafasi ya kufurukuta mbele ya Yanga wakipachika dakika ya 65 kupitia kwa Meddie Kagere.
Kibwana amesema:”Nilikuwa nina nia ya kufunga kabla ya mchezo na imefanikiwa na imekamilika, hili ni goli langu la kwanza nimefurahi na ninamshukuru aliyenipa pasi.
“Mayele amenipa psi ninamshukuru ninasema asante kwa ajili ya hilo kafanya jambo kubwa na tutazidi kupambana,” amesema.
Yanga inafikisha mchezo wa 47 bila kufungwa ndani ya ligi tangu ilipopoteza mbele ya Azam FC msimu wa 2021/22.