>

SIMBA YAMTAMBULISHA KOCHA WA VIUNGO

RAMSI Kelvin Mandla kutoka Afrika Kusini ametambulishwa kuwa  kocha wa viungo (Fitness Coach).

Kabla ya kocha huyo Simba haikuwa na kocha wa viungo baada ya aliyekuwa kweye nafasi hiyo kuondoka.

Anakuwa kocha wa pili kutambulishwa kwenye benchi la ufundi ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda.

Novemba 15,2022 Simba ilimtamulsha kocha wa makipa raia wa Morocco ambaye ni Chlouha Zakaria.