HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA

 LIGI Kuu Tanzania Bara leo Novemba 16,2022 inaendelea kwa timu kuyeyusha dakika 90 kusaka pointi tatu.

Mtibwa Sugar ambayo imetoka kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Azam FC kwa kukubali ubao wa Uwanja wa Manungu usoma Mtibwa Sugar 3-4 Azam FC inakwakaribisha Coastal Union, Uwanja wa Manungu.

Tanzania Prisons wao watakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Geita Gold ambao nao wanahitaji pointi tatu hizo.

Simba ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Ihefu inawakaribisha Namungo ambao wametoka kupoteza kw kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.