RONALDO: MANCHESTER UNITED IMENISALITI

CRISTIANO Ronaldo amebainisha kuwa Klabu ya Manchester United imemsaliti kwa kuwa wanamlazimisha aondoke.

Ronaldo amefunguka hayo kwenye mahojiano maalumu na gwiji wa habari, Piers Morgan.

Kabla ya msimu wa 2022/23 kuanza iliripotiwa kuwa nyota huyo anataka kusepa ndani ya Manchester United baada ya timu hiyo kushindwa kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Nyota huyo amesema:”Manchester United wamenisaliti mimi. Nahisi kuwa kuna watu walikuwa hawanitaki ndani ya United na sio kocha pekee na watu wengine na hii sio mwaka huu tu hata msimu uliopita.

“Kwa sasa sina heshima mbele ya Erik ten Hag sababu yeye ameshindwa kunionyesha heshima na kama huna heshima na mimi siwezi kuwa na heshima na wewe,”.