>

AZAM FC WANAWAKA MANUNGU

AZAM FC wanaongoza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar unaochezwa uwanja wa Manungu, Moro.

Kasi ya Azam FC ilianza kipindi cha kwanza ambapo walipata mabao yote hayo matatu yaliyowapa uongozi.

Ni Idris Mbombo ambaye ametupia mabao mawili dakika ya 18 na 30 kwenye mchezo huo wakiwa ugenini.

ao la tatu ni mali ya Abdalah Kheri ambaye amefunga dakika ya 41 chini ya Kaimu Kocha Kali Ongala.

Mchezo uliopita Azam FC ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar ilitoka kufungwa mabao 5-0 dhidid ya Simba.