BAYERN Munich inaamini kwamba jeraha ambalo amepata Sadio Mane sio kubwa sana kuelekea kwenye Kombe la Dunia ingawa kwa sasa wanasubiri vipimo.
Mane aliumia juzi wakati wa mchezo wa Bundesliga dhidi ya Werder Bremen na kuibuka na ushindi wa mabao 6-1.
Kwa maumivu aliyopata nyota huyo aliondolewa uwanjani katika mchezo huo na sasa zimesalia siku 10 pekee kabla ya Kombe la Dunia kuanza.
Winga huyo matata aliumia dakika 15 za mwanzo za mchezo huo na kutolewa uwanjani na nafasi yake ilichukuliwa na Leroy Sane.
Mane anatakiwa kuwa mmoja wa wachezaji wa Senegal kutoka Afrika kwenda kuwakilisha katika Kombe la Dunia nchini Qatar ambapo kuumia kwake ni kama kumezua hofu.
Kocha wa timu hiyo Julian Nagelsmann amesema:”sikuweza kuonana naye mara baada ya mechi lakini ninaamini hajapata tatizo kubwa tunasubiri ripoti ya daktari kujua tatizo likoje,”,