VIJANA wa Brighton wameibuka na ushindi wakiwa ugenini dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Carabao.
Ubao ulisoma Arsenal 1-3 Brighton na kuwafanya wawaondoe Arsenal kwenye kuwania taji la Carabao.
Ni mabao ya Danny Welbeck dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti, Kaoru Mitoma dakika ya 58 na Tariq Lamptey dakika ya 71.
Bo pekee la Arsenal walipachika dakika ya 20 kupitia kwa Eddie Nketiah dakika ya 20 wakiwa Emirates.
Rekodi zinaonyesha kwamba ni mashuti 22 Arsenal walipiga huku Brighton wakipiga mashuti 13 na timu zote mashuti manne yalilenga lango