MADRID NA LIVER FAINALI YAO IMEBUMA

MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid wataanza ugenini dhidi ya Liverpool na wababe PSG watavaana na Bayern Munich kwenye mechi za hatua ya 16 bora.

Mechi za raundi hiyo zinatarajiwa kuanza kupigwa Februari 14 mpaka Machi 14, mwakani 2023 baada ya droo kuchezwa Novemba 7,2022.

Liverpool na Real Madrid msimu uliopita zilikutana hatua ya fainali ambapo Liverpool ilinyooshwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Vinicius Junior.

Ilikuwa ni rekodi ya tatu kwa wababe hao kukutana kwenye fainali za Ulaya lakini msimu huu mambo yamebuma mapema kabisa.

Mechi nyingine ni Borussia Dortmund v Chelsea, RB Leipzig v Manchester City,Inter Milan v FC Porto, Frankfurt v Napoli, AC Milan v Tottenhamna Club Brugge v Benfica.

Kwenye Europa League hatua ya mtoano Manchester United wamepangwa kucheza dhidi ya Barcelona. Pia Juventus v Nates, Sporting CP v Midtjylland, Shakhatar Donetsk v Rennes, Ajax v Union Berlin, Bayer Leverkusen v Monaco, Sevilla v PSV Eindhoven na Red Bull Salzburg v AS Roma