IAN Wright, mkongwe wa Arsenal amekiri kuwa ana hofu juu ya Bukayp Saka kuwa anaweza kupata majeraha kuelekea Kombe la Dunia.
Saka aliumia hivi karibuni na sasa amepana na leo atakuwa sehemu ya mchezo wa London Dabi dhidi ya Chelsea.
Winga huyo awali aliumia kwenye mchezo kati ya Arsenal na Nottingham Forest wakati Arsenal wakishinda mabao 5-0.
England tayari ina wachezaji ambao ni majeruhi ikiwa ni pamoja na Reece James na Ben Chilwell.
Wright anaamini Saka amekuwa akikamiwa zaidi na wapinzani, huku kocha wake Mikel Arteta akishindwa kumpumzisha kutokana na kukosa wachezaji wa aina yake.
“NI huzuni kuona watu wa Arsenal wakisema (Saka) apumzishe kwa sasa lakini ni lazima aipambanie timu yake.
“Tuliona jinsi Saka alivyoumia dhidi ya Nottingham, alitoka kwa huzuni kama ilivyokuwa kwa Varane, (Raphael) alilia kwa sababu alijua nini kipo mbele yake.
“Nafikiri kama Emile Smith Rowe angekuwa fiti basi Saka angepumzika. Ila hali ipo tofauti .Kwa sasa Saka akiumia inakuwa ni hofu sababu Kombe la Dunia lipo njiani anahitajika katika kikosi,”.