WOLVERHAMPTON Wanderers imemtambulisha rasmi Julen Lopetegui raia wa Hispania na aliyewahi kuwa Kocha mkuu wa Klabu ya Real Madrid pamoja na Sevilla kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.
Lopetegui hivi karibuni ametimuliwa kazi kutoka Klabu ya Sevilla anaanza kuwa kwenye majukumu yake mapya kwenye timu hiyo.
Lopetegui anachukua mikoba ya Bruno Lage ambaye alitimuliwa klabuni hapo Oktoba 2 baada ya kushinda mchezo mmoja tu kati ya michezo yake 15 ya mwisho.
Klabu ya Wolves imekuwa ikipitia kipindi kigumu cha matokeo uwanjani licha ya timu hiyo kuwa na nyota wengi akiwepo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Atletico Madrid Diego Costa.