NYOTA wa timu ya Taifa ya Ujerumani na Klabu ya RB Leipzig ya nchini humo ambaye amewahi kukipiga katika klabu ya Chelsea Timo Werner, huenda akakosekana katika michuano ya Fainali za Kombe la Dunia 2022 zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Novemba 21.
Werner alipata majeraha ya kifundo cha mguu katika mchezo wa mwisho wa hatua za makundi ya klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) dhidi ya Klabu ya Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine.
Baada ya mchezo huo vipimo vya Scan vilibainisha kuwa Werner anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa zaidi ya wiki nane ambayo ni sawa na miezi miwili.
Baadhi ya nyota wengine ambao nao wapo kwenye hatihati kukosa mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar ni pamoja na Reece James wa Chelsea, Son Heung Min wa Totenham Hotspurs, Ben Chilwell, Paul Pogba pamoja na Ngolo Kante.