>

KIUNGO WA KAZI CHELSEA KUSEPA BURE

KIUNGO wa klabu ya Chelsea Ngolo Kante ameripotiwa huenda akaondoka klabuni hapo bure kabisa mwishoni mwa msimu ujao kutokana na kumalizika kwa mkataba wake na kutokuwepo kwa maendeleo yoyote kwenye mazungumzo ya mkataba mpya.

Kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa Habari za michezo Fabrizio Romano amebainisha kuwa upo uwezekano mkubwa wa kiungo huyo raia wa Ufaransa kutimka klabuni hapo kutokana na wakala wake pamoja na klabu ya Chelsea kutofikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya kwa mchezaji huyo.

Kante ambaye amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara na ya muda mrefu yupo nje akiuguza majeraha ambayo yanatarajiwa kumuweka nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu hali iliyopelekea kuondolewa kwenye mipango ya kushiriki katika Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwishoni mwa mwezi ujao.

Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania inapewa chapuo kubwa la kuwa sehemu ambayo Kante anaweza kutimkia huku vilabu vingine vikubwa kama Paris Saint German pamoja na baadhi ya vilabu vinavyoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza navyo vikielezwa kuonesha nia ya kumsajili nyota huyo.