>

WANNE WA SIMBA KUIKOSA AZAM FC LEO KWA MKAPA

MASTAA wanne wa Simba wanatarajia kuukosa mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC kutokana na sababu mbalimbali.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda leo Oktoba 27,2022 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mgunda ameweka wazi kuwa maandalizi kwa ajili ya mchezo wa leo yapo sawa lakini watakosa huduma za nyota wake kutokana na sababu mbalimbali.

“Yupo Israel Mwenda huyu alipata maumivu kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga pia Jimson Mwanuke na Sadio Kanoute hawa bada hawajawa fiti kutokana na kupata maumivu hivi karibuni.

“Lakini pia Mzamiru Yassin huyu kutokana na kanuni yeye ana kadi tatu za njano hivyo hataweza kuwa sehemu ya kikosi kwa kuwa anatumikia adhabu hiyo lakini wengine wapo tayari.

“Shomari Kapombe amerejea tayari na ameanza mazoezi na wachezaji wenzake hivyo tuwaombee wachezaji wetu waamke salama, washinde salama ili wakapate pointi tatu mbele ya Azam FC,” .