TIMU ya Wanawake, ya Simba Queens imeingia mkataba wa udhamini wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubashiriki ya M Bet wenye thamani ya Tsh. bilioni moja.Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mkataba huo hauingiliani na mkataba wa timu ya wanaume.Sababu kubwa za kuweza kupata udhamini huo ni kutokana na kufanya vizuri kwa timu hiyo ya Wanawake ambayo imetwaa ubingwa wa ligi ya Wanawake Tanzania mara nne.”Huu ni mkataba wa kipekee na hauna uhusiano na ule wa timu ya wanaume hivyo hii nayo ni tasisisi ambayo inajitegemea nao mkataba wao unajitegemea ni jambo kubwa na furaha kuona kwamba hata timu ya Wanawake nayo inakuwa na udhamini mkubwa.Barbra Gonzalez Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa ni furaha kuona jambo la kihistoria linafanikiwa na wanawakaribisha wengine kuendelea kudhamini.”Huu ni mwanzo na ni mkataba mkubwa na mzuri nadhani haujawahi kutokea kwa hivi karibuni kwa upande wa Wanawake, ilioni moja kwa muda wa miaka mitano sio jambo dogo.
“Kila mwaka ni milioni 200 zitakuwa zinatolewa hii inamaanisha kwamba Simba ni taasisi kubwa na kila watu ambao wanawekeza hapa wanapata faida,” amesema.Simba Queens itaanza kutumia jezi zenye nembo ya M-Bet kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.