SIMBA KUPATA ADHABU KISA MECHI YA YANGA

KLABU ya Simba SC inasubiri adhabu kutoka katika Bodi ya Ligi Kuu Bara kwa sababu ya kufikisha kadi za njano tano (5) katika mchezo mmoja ambazo ni kinyume na kanuni.

Katika mchezo wa Oktoba 23, 2022, Derby ya Kariakoo, klabu ya Simba SC imepata kadi za njano tano huku watani wao wa jadi, Klabu ya Yanga SC ikipata kadi za Njano nne (4).

Mwamuzi wa mchezo, Ramadhani Kayoko ametoa kadi za njano 9 kama ifuatavyo;

Okra Augustine (Simba)

Feisal Salum (Yanga)

Mzamiru Yassin (Simba)

Mohamed Hussein (Simba)

Khalid Aucho (Yanga)

Aziz Ki (Yanga)

Jonas Mkude (Simba)

Djuma Shabani (Yanga)

Habib Kyombo (Simba).