MANCHESTER United wanatamba na ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Tottenham na kusepa na pointi tatu muhimu.
Mchezo huo mkali ulichezwa Uwanja wa Old Trafford, mabao ya Fred dakika 47 na Bruno Fernandes dakika ya 69.
Ni jumla ya mashuti 28 Man U walipiga huku Tottenham wakipiga mashuti 9.
Kati ya hayo United ni mashuti 10 huku wapinzani wao wakipiga mashuti mawili.
Ushindi huo unawafanya United kuwa nafasi ya 5 na pointi 19 huku Tottenham wakiwa nafasi ya 3 na pointi 23.