UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hauna mpango wa kumfuta kazi Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kwa kuwa bado wanamtambua kuwa ni kocha wa timu hiyo.
Imekuwa ikielezwa kuwa kwa kushindwa kuipeleka Yanga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ni sababu ya kocha huyo kuwa kwenye mtego wa kutimuliwa.
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa bado wanamtambua Nabi kuwa ni kocha wa timu hiyo na hawana mpango wa kumfukuza.
“Taarifa ambazo zinasambazwa hizo hazina ukweli kwama tunahitaji kumfukuza Nabi, ambacho kipo ni kwamba yeye bado ni kocha wa Yanga na anaendelea na majukumu yake,” amesema.