FISTON Mayele ametupia mabao matatu ndani ya ligi akiwa sawa na mzawa Feisal Salum.
Nyota huyo anawania kiatu cha ufungaji bora ambacho alipishana nacho msimu wa 2021/22 kilipobebwa na mzawa George Mpole.
Mayele alitupia mabao 16 kwenye ligi msimu uliopita huku Mpole akitupia mabao 17 na wote walitoa pasi nne za mabao.
Ni dakika ya 41 alifunga dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, dakika ya 67 mbele ya Coastal Union, bao la tatu dakika ya 38 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa.
Mabao mawili kafunga kipindi cha kwanza na moja kipindi cha pili kwenye ligi msimu huu wa 2022/23.
Nyota huyo amesema kuwa wanazidi kupambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye timu hiyo inayonolewa na Nasreddine Nabi.
“Muhimu kila mmoja kutimiza majukumu yake ni wakati wetu wa kuendelea kupambana kupata matokeo na ushindani ni mkubwa,”.