JOE Gomez huenda akaitwa timu ya taifa ya England kwa ajili ya Kombe la Dunia mwezi ujao.
Beki huyo wa Liverpool alikuwa kwenye ubora wakati timu hiyo ikiichapa Man City bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
Kwa mujibu wa Daily Mail inaaminika kwamba ataitwa katika kikosi cha wachezaji 26 na kocha Gareth Southgate kufuatia majeraha ya Reece James.
Gomez mwenye miaka 25 hajaichezea England kwa miaka miwili baada ya kupata majeraha makubwa mazoezini akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa.
Ni mechi 11 amecheza chini ya kocha Southgate ambaye anatajwa kukubali uwezo wa beki huyo.