BAADA ya kupoteza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal, kikosi cha Yanga leo kimeanza safari ya kurejea Tanzania.
Msafara huo ambao uliongozana na viongozi utapitia Addis Ababa Ethiopia.
Bado Yanga inabaki kwenye anga za kimataifa kwa kuwa imeangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrka.
Inafanya zibaki timu mbili Tanzania ambazo zinapeperusha bendera ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Simba.
Azam FC na Kipanga wao jitihada zao ziligota mwisho baada ya kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zao ambazo walicheza.
Azam licha ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Al Akhadar ya Libya imeondolewa kwa jumla ya mabao3-2 kwa kuwa mchezo wa ugenini ilipoteza huku Kipanga wenyewe wakiondolewa kwa jumla ya mabao 7-0 dhidi ya Club Aficain.