YANGA YAPOTEZA DHIDI AL HILAL KIMATAIFA

KIKOSI cha Yanga kimekwama kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa nguvu zao ni kwenye Kombe la Shirikisho.

Kwenye mchezo wa leo dhidi ya Al Hilal walikubali kupoteza kw bao 1-0 Yanga.

Ni bao la dakika ya 3 lilitosha kuwapa ushindi Al Hilal wakiwa nyumbani na kutinga hatua ya makundi.

Mohamed Abdrahaman alipachika bao hilo akiwa ndani ya 18 na kuipa ushindi Al Hilal.