MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa akili zao kwa sasa zinafikiria mchezo wa leo dhidi ya de Agosto ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda ina kibarua cha kulinda ushindi wa mabao 3-1 ilioupata nchini Angola ili kuweza kusonga mbele katika hatua ya makundi.
Ally amesema:”Kila mmoja anatambua kwamba kwa sasa tunakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya de Agosto akili zetu tumezielekeza huko ili kupata matokeo mazuri.
“Tulishinda lakini bado hatujafuzu, safari hii hatutaki kurudia makosa. Tumeweka nguvu kubwa kuona kwamba mchezo wa Jumapili tunapata matokeo mazuri ili tuingie makundi. Tumemiss kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”
“Tutaendelea kuwakosa Shomari Kapombe ambaye sasa anaendelea kufanya mazoezi akiwa hospitali, ataukosa mchezo wa Jumapili lakini michezo itakayofata atakuwepo. Jimmyson Mwinuke pia tutamkosa, taarifa njema ni Peter Banda amerejea kikosini.”