LIVERPOOL YAKOMBA POINTI TATU ZA CITY

MOHAMED Salah mshambuliaji wa Liverpool amefunga bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Man City.

Ni bonge moja ya mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa ambapo dakika 45 vigogo hao walikamilisha bila kufungana.

Salah alipachika bao hilo dakika ya 76 lilitosha kuipa pointi tatu muhimu Liverpool.

Sasa ni pointi 13 wanafikisha huku City wakibaki na pointi 23 kibindoni ni Uwanja wa Anfield mchezo umechezwa.