MBEYA CITY YAINYOOSHA POLISI TANZANIA

KIKOSI cha Polisi Tanzania kimeadhibiwa na nyota wa Polisi Tanzania ambao walikuwa kwenye kikosi hicho kwa nyakati taofauti na sasa wanapata changamoto mpya ndani ya Mbeya City.

Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine, baada ya dakika 90, ubao umesoma Mbeya City 3-1 Polisi Tanzania.

Ni mabao ya Hassan Nassoro dakika ya 50, Sixstus Sabilo dakika dakika ya 64 na Tariq Seif dakika ya 73 yalitosha kuipa ushindi Polisi Tanzania.

Kwa upande wa Polisi Tanzania ni bao la Vitalis Mayanga hili lilikuwa lakufutia machozi dakika ya 16 licha ya wao kutangulia ngoma haikuwa upande wao kwenye mlio mzuri.